Timu ya taifa ya Rwanda, Amavubi Stars inasaka tikiti ya kufuzu kwenye michuano ya Afcon 2022. Kesho Jumanne ina mtihani dhidi ya Simba wanyika Cameroon mjini Duala. Ni mchuano unaosubiriwa na wengi kujua hatma ya Timu ya Rwanda kama itafuzu au la.
Kocha mkuu wa Timu ya Rwanda Mashami Vicent baada ya kuichapa Msumbiji bao 1-0 mjini Kigali wiki jana, aliondoka ijumaa na kikosi cha wachezaji 23 kuelekea Cameroon kujiandaa kumenyana na Simba wa Nyika hapo kesho mjini Duala.
Miongoni mwa wachezaji waliorejea ni pamoja na mlinda mlango wao Olivier Kwizera ambaye hakucheza mechi ya Msumbiji kutokana na kadi nyekundu aliyopewa katika mchuano ya hatua ya ¼ fainali ya kombe la CHAN 2021 dhidi ya Guinea.
Kocha mashami Vicent ameomba wanyarwanda msaada wa maombi ili washinde mechi hii muhimu dhidi ya Cameroon.
Katika kundi hili la F, Cameroon wanaongoza na alama 10, Cape Verde iko kwenye nafasi ya pili na alama 7, Rwanda kwenye nafasi ya 3 na alama 5 wakati Msubiji ikiwa na alama 4. Endapo Cape verde watashinda mechi ya ugenini dhidi ya Msumbiji, Rwanda hata ikifunga Cameroon itayaaga mashindano hayo ikifuata Tanzania na Kenya.
Ni michuano inayotarajiwa kuchezwa mwezi januari na Februari mwakani nchini Cameroon.
Rwanda ilifuzu kucheza michuano hiyo mwaka 2004 nchini Tunisia. Kama inaweza kurejea kwa mara ya pili katika fainali za AFCON 2021 nchini Cameroon.