Inter yashinda derby ya Milan na kukamata nafasi ya tatu

Kabla hata ya mtanange wenyewe kuanza, ilibainika wazi kuwa Derby della Madonnina iliweka rekodi mpya katika ligi ya Italia – Serie A kwa kuingiza mapato ya euro milioni 5.7 katika mauzo ya tiketi na kitalii.

Zaidi ya tiketi 4,000 zilinunuliwa na mashabiki wa nje ya Italia na wamesafiri kwa ajili tu ya derby hiyo maarufu kama #DerbyMilano. Na baada ya mechi kukamilka uwanjani San Siro, ni dhahiri kuwa mashabiki waliofika uwanjani waliondoka wakiwa na tabasamu.

Bakayoko alifunga bao safi la kichwa na kuirejesha Milan mchezoni

Mtanange huo kati ya watani wa jiji AC Milan na Inter Milan ulikuwa na kila aina ya uhondo. Mwishowe, Inter iliibuka na ushindi na kuwapiku AC Milan katika nafasi ya tatu ya Serie A kwa ushindi wa kusisimua wa 3-2.

Bao la Matias Vecino liliwapa Nerazzurri uongozi uliostahiki kabla ya kipindi cha mapumziko kabla ya Stefan De Vrij na Lautaro Martinez, kupitia penalti, kufunga baada ya kipindi cha pili, wakati mabao kutoka kwa wachezaji wa Milan Tiemoue Bakayoko na Mateo Musacchio kuwarejesha Rossoneri mchezoni.

Inter wamefikisha mechi sita za derby ya Milan bila kupoteza hata moja na sasa wamewaruka watani wao hao hadi nafasi ya tatu na pointi 53, mbili juu ya Milan katika nafasi ya nne.

Ospina aliondolewa uwanjani baada ya kuzimia

Nambari mbili kwenye ligi Napoli waliponea mapambano ya Udinese na kushinda 4-2 lakini kulikuwa na hofu ya kipa David Ospina kupata jeraha la kichwa.

early in the game and collapsed later in the first half before being carried off on a stretcher and taken to hospital.

Imeripotiwa kuwa uchunguzi wa kichwa umeonyesha yuko sawa lakini ataangaliwa kwa siku mbili zaidi.

Napoli wamepunguza pengo kati yao na vinara Juventus hadi pointi 15.

Juventus – bila ya shujaa wake wa Champions League Cristiano Ronaldo – walipata kipigo cha kwanza cha msimu katika Serie A walipozabwa 2 – 0 dhidi ya Genoa.

Author: Bruce Amani