Southgate azawadiwa mkataba mpya

Gareth Southgate amesaini mkataba mpya wa kuendelea kuwa kocha wa timu ya kandanda ya England hadi Kombe la Dunia 2022.

Southgate ambaye mkataba wake wa awali ulistahili kumalizika baada ya dimba la Euro 2020, aliwaongoza the Three Lions hadi nusu fainali ya Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika miaka 28 mwaka huu nchini Urusi.

Mshahara wake sasa unaripotiwa kuongezeka hadi pauni milioni tatu wa mwaka.

“Nna furaha kuwa na fursa ya kuiongoza timu ya taifa katika mashindano mawili makuu yajayo”. Amesema Southgate. Naibu wake Steve Holland pia amekubali mkataba mpya hadi mwaka wa 2022.

Author: Bruce Amani

EnglandGareth Southgate