Tanzania yaanza vibaya Afcon kwa kuzabwa na Senegal

Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars imeangukia pua kwa kupoteza mchezo wa kwanza wa michuano ya Kimataifa Afrika AFCON baada ya kukubali kipigo cha goli 2-0 dhidi ya Senegal, mchezo wa kundi C.

 

Tanzania ikiwa chini ya Kocha Emmanuel Amunike ilianza kupoteza uelekeo kunako dakika ya  27 baada ya Keita Balde kuitanguliza Senegal kabla ya kufungwa goli lingine kipindi cha pili kupitia kwa K. Diatta kwa shuti kali.

Mpaka dakika 90 zinamalizika Tanzania 0-2  Senegal. Mchezo wa pili kwa Tanzania utafanyika Alhamis dhidi ya majirani zao Kenya ukiwa muendelezo wa mashindano hayo.

Mechi inayofuata leo Jumapili Kenya vs Algeria.

Author: Bruce Amani