Bayern Munich, Dortmund na Leipzig waibuka kidedea Bundesliga

Pale alipoishia ndipo alipoanzia, suala la kufunga kwake ni suala la muda pekee si mwingine bali ni Robert Lewandowski mshambuliaji wa Bayern Munich ambaye amekuwa na mfululizo wa mafanikio katika kuzifumania nyavu. Katika mtanange wa leo Lewandowski ametupia bao mbili wakati Bayern ikitoa adhabu ya bao 4-1 dhidi ya Arminia Bielefeld.

Strika huyo wa kimataifa wa Poland amefunga goli 102 katika mechi 100 ndani ya Bayern Munich. Magoli mawili mengine amefunga Thomas Muller, kabla ya Ritsu Doan kufunga la kufuatia machozi kwa upande wa Arminia. kiungo wa Bayern Corentin Tolisso alionyeshwa kadi ya moja kwa moja nyekundu katika mechi hiyo

Bayern wametoshana pointi na Borrusia Dortmund ambao mapema siku ya leo wamepata matokeo ya goli 1-0 dhidi ya Hoffenheim. Goli hilo lilifungwa na nahodha wa kikosi hicho Marcus Reus.

Katika matokeo mengine RB Leipzig walipata ushindi wa mabao mawili kwa sifuri dhidi ya Augsburg

Author: Bruce Amani