Bayern waendeleza ubabe Bundesliga, waifunga Augsburg 1-0

Mshambuliaji wa kimataifa wa Poland Robert Lewandowski ameendelea kuipa ushindi timu yake ya Bayern Munich baada ya kufunga goli pekee na la ushind katika mechi hiyo huku Bayern wakiendelea kutawala maisha ya kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Ujerumani.

Goli la Lewandowski lilipatikana kwa njia ya penati baada ya mwamuzi kuamuru kupigwa kwa tuta . Hata hivyo Augsburg wangeweza kusawazisha kwa njia ya penati lakini mpira wa Alfred Finnbogason uligonga mwamba na kukosa tuta hilo.

Lewandowski linakuwa bao lake la 22 kwenye Ligi pekee zikiwa ni takwimu za aina yake, akiwa amefunga goli 12 katika mechi 11 ndani ya Bavarian hao.

Ushindi unaifanya Bayern kubakia kileleni huku RB Leipzig wakiwa nafasi ya pili baada ya kushinda 1-0 pia dhidi ya Union Berlin na kuwatoa Bayer Leverkusen.

Author: Asifiwe Mbembela