PSG yatawala Ufaransa hata bila ya Neymar

Kocha wa Paris Saint-Germain Thomas Tuchel amesema Marco Verratti na Angel Di Maria bado wanaweza kushiriki katika mchuano wao wa Champions League dhidi ya Napoli. Verratti na Di Maria waliondoka uwanjani wakati PSG iliibamiza Amiens 5-0 katika mpambano wa Ligue 1 ya Ufaransa

PSG iliendeleza matokeo yake ya ushindi katika msimu huu wa ligi hadi mechi 10 huku mabao yake yakifungwa na wachezaji Marquinhos, Adrien Rabiot, Julian Draxler, Kylian Mbappe na Moussa Diaby. Bao la Mbappe lilikuwa lake la 11 msimu huu katika ya mechi tisa.

Tuchel aliweza kumpumzisha Neymar baada ya kushiriki katika mchuano wa Brazil dhidi ya Argentina siku nne zilizopita. PSG imejiimarisha kileleni na pointi 30 ikifuatwa na Lille na pointi 22 baada ya kuichapa Dijon 2-1.

Author: Bruce Amani

PSGThomas Tuchel