Tanzania, Kenya zatolewa Afcon 2021, timu 14 zakanyaga Cameroon

Wakati timu nyingine zikitolewa na kupoteza nafasi ya kushiriki michuano ya fainali ya Kombe la Mataifa Bingwa Afrika Afcon 2021 kama Kenya na Tanzania, tayari timu 14 zimefuzu na kubakiwa na timu 10 pekee kutafuta nafasi hizo.

Fainali za mwaka huu zitafanyika nchini Cameroon kufuatia mwaka Juzi kufanyika Misri katika zamu ya Cameroon baada ya taifa hilo kushindwa kukamilisha baadhi ya taratibu za maandalizi za michuano hiyo mkubwa ngazi ya taifa.

Kwenye timu hizo 14 ambazo tayari zimefuzu, timu mbili zitaenda kucheza mashindano hayo kwa mara ya kwanza ambayo ni Visiwa vya Comoros, na Gambia.

Mbali na Cameroon wenyeji, timu nyingine ambazo zimefuzu ni Algeria mabingwa watetezi, Burkina Faso, Egypt, Equatorial Guinea, Gabon, Ghana, Guinea, Mali, Senegal (wanafainali), Tunisia, Zimbabwe.

Bado timu pekee 10 pekee kukamilisha nchi ambazo zitashiriki fainali hizo.

Author: Asifiwe Mbembela