Yanga kuangushana na Biashara hatua ya 32 bora Kombe la Shirikisho

Shirikisho la Soka Tanzania {TFF} limefanya droo ya michuano ya Kombe la Shirikisho maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) hatua ya 32 bora huku mabingwa wa kihisoria wa ligi kuu ya Tanzania Young Africans wakipangwa na timu ya Biashara United na mshindi katika mchezo huo atavaana na mshindi kati ya Mighty Elephant na Namungo FC katika hatua ya 16 Bora ya michuano hiyo kuelekea robo fainali.

Mabingwa watetezi wa taji, Walima Miwa wa Manungu Morogoro Mtibwa Sugar watajaribu kutetea kombe lao kwa kupambana na wana Lizombe Maji Maji FC ya Songea, na mshindi katika mchezo huu atapata fursa ya kuvaana na mshindi kati ya KMC na Pan Africans

Nao waoka mikate wa Azam FC watamenyana na Pamba SC ya Mwanza moja ya timu yenye historia kubwa katika soka la Bongo na mshindi wa hapa atajipanga kukutana na mshindi kati ya Rhino Rangers na Stand United.

Vigogo hawa wote watatu yaani Yanga, Azam na Mtibwa watacheza michezo hiyo katika viwanja vyao vya nyumbani. Mechi zote za Raundi ya Nne, ya michuano hii zitafanyika kati ya Januari 25 na 28, na  hatua ya 16 Bora inataraji kupigwa Februari 22 na 25 na Robo Fainali zitafanyika kati ya Machi 27 na 30 wakati fainali ya michuano hiyo mwaka huu itafanyika Uwanja wa Lulu mjini Lindi

RATIBA HATUA YA 32 BORA ASFC
Yanga SC V Biashara United
Mtibwa Sugar V Maji Maji FC
Azam FC V Pamba SC
Mashujaa FC V Mbeya City FC
Friends Rangers V African Lyon
Mighty Elephant V Namungo FC
Alliance FC V La Familia
Dodoma FC V Transit Camp
Cosmo Politan V Dar City
Reha FC V Boma FC
Rhino Rangers V Stand United
KMC V Pan Africans
Kagera Sugar V Mbeya Kwanza
Polisi Tanzania V Lipuli FC
Kitayose V Coastal Union
Singida United V JKT Tanzania
(Mechi zote zitafanyika kati ya Januari 25 na 28, 16)

Author: Bruce Amani