Mabao mawili ya Gervinho yaiduwaza Juventus

Juventus inavuja mabao na kocha Massiialiano Allegri ana wasiwasi kabla ya mchuano wa Champions League hatua ya 16, ambapo watakutana na Atletico Madrid. Kwa mara ya pili katika wiki moja, Juventus imefungwa mabao matatu wakati Parma ilitoka nyuma 3 – 1 na kupata sare ya 3 – 3 mjini Turin katika mchuano wa Serie A Jumamosi.

 

Haa mabao mawili ya Cristiano Ronaldo hayangeweza kuisaidia Juventus kushinda. Vinara hao wa Serie A wameshuhudia uongozi wao ukipunguzwa hadi pointi tisa dhidi ya nambari mbili Napoli, ambayo hapo mapema iliizaba Sampdoria 3 – 0.

 

Ilikuwa ni mara ya kwanza katika miaka saba ambapo Juventus hawakuweza kumtegemea yeyote kati ya safu yake ya ulinzi ya BBC inayowajumuisha Andrea Barzagli, Leonardo Bonucci na Giorgio Chiellini — kwa sababu wote watatu ni majeruhi. Mabao ya Parma yalifungwa na Antonino Barilla na Gervinho aliyefunga mawili

 

Mabao ya Napoli yalifungwa na Lorenzo Insigne, Arkadiusz Milik na Simone Verdi.

Author: Bruce Amani