Tetesi za Mastaa Ulaya: Manchester United waingilia dili la Chelsea kwa fundi wa West Ham United

Manchester United watatuma ofa kwenda kwa kiungo mkabaji wa West Ham United Declan Rice 21 licha ya nyota huyo wa England kuonekana kama anampenzi na klabu ya Chelsea.

Wolves wanamtazama mshambuliaji wa kimataifa wa Ubeligiji Liverpool Divock Origi, 25, ambaye mkataba wake unamruhusu kuondoka Liverpool hata katika dirisha dogo la usajili la mwezi Januari.

Manchester United wako kwenye mchakato wa kumwachia beki wao Marcos Rojo, 30, mwezi Januari, wakati ambao klabu ya Newcastle United inahitaji huduma ya mlinzi huyo kwa mkopo.

Kocha mpya wa kikosi cha West Bromwich Albion Sam Allardyce ameweka kipaumbele chake kwenye kulifumua eneo la ulinzi la klabu hiyo, ambapo beki wa Crystal Palace James Tomkins, 31, amekuwa chaguo lake la kwanza.

Mgombea anayewania Urais katika klabu ya Barcelona Victor Font amesema hata toa ahadi za kusajiliwa mastaa klabuni hapo kama ambavyo baadhi ya wagombea wamekuwa wakisema, yeye(Victor) atahakikisha staa na nahodha wa timu hiyo Lionel Messi, 33, anaongeza mkataba mpya.

Author: Bruce Amani