Bandari FC Yavuna pointi moja kwa Gor Mahia

328

Bandari FC imeambulia alama moja baada ya kuilazimisha sare ya goli 1-1 na Gor Mahia katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Kenya KPL mchezo uliopigwa Jumapili.

Kwenye mechi hiyo, Mahia walikuwa wanahitaji kushinda ili kukwea mpaka nafasi ya nne kwenye msimamo wa KPL hata hivyo wamepoteza nafasi kutokana na sare waliyoipata jioni kabisa kwa Bandari kusawazisha.

Magoli ya timu zote mbili yamefungwa na wachezaji ambao ni raia wa Uganda Peter Lwasa (Gor Mahia) na William Wadri (wa Bandari) wakiwa ni wachezaji raia wa Uganda.

Sare hiyo inakuwa ya kwanza kwa kocha wa muda wa Anthony ‘Modo’ Kimani baada ya kuichukua timu hiyo kutoka kwa Andre Casa Mbungo kufuatia matokeo mabaya.

Bandari wanakwea mpaka nafasi ya saba.

Author: Bruce Amani