Simba watua Dar kutoka Zambia

260

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu nchini Tanzania, klabu ya Simba SC wamerejea Jijini Dar es Salaam kwa maandalizi ya mwisho kuelekea mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara dhidi ya Watani wao wa Jadi, Yanga Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Simba ilikuwa Zambia tangu Ijumaa ambako walikwenda kumenyana na wenyeji, Red Arrows katika mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika, ambao walifungwa 2-1 Jumapili, lakini wamefuzu hatua ya makundi kwa ushindi wa jumla wa 4-2 kufuatia kushinda 3-0 kwenye mchezo wa kwanza Dar es Salaam.

Wakati wakisubiri kurejea nchini klabu hiyo iliendelea na mazoezi huko huko Lusaka ambapo wachezaji kadhaa waliungana na timu hiyo akiwemo Chris Mugalu na Tadeo Lwanga ambapo kwa mjibu wa Kaimu Afisa Habari wa Simba amesema kuwa wachezaji hao wako fiti linabakia chaguo la kocha

Author: Asifiwe Mbembela