Tetesi za Mastaa Ulaya: Mkataba wa miaka mitano wa Messi kutangazwa karibuni, Ofa ya Man City kwa Kane yatupiliwa mbali

202

Manchester City imepungukiwa na kiasi cha pauni milioni 40 ili kufikia pauni milioni 160 ambayo klabu hiyo Tottenham Hotspur inahitaji kwa ajili ya kumuuza mshambuliaji wake Harry Kane, 28.

Chelsea bado hawajakata tamaa ya kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Ubeligiji na Inter Milan Romelu Lukaku 28, licha ya mchezaji huyo kuonekana hajaridhia kutoka Milan

Barcelona watatangaza mkataba mpya wa staa wa Argentina Lionel Messi 34, mkataba huo unategemewa kuwa wa miaka mitano.

Newcastle United wako kwenye mazungumzo na klabu ya Juventus ili kuangalia uwezekano wa kumsajili kiungo mshambuliaji wa Wales Aaron Ramsey, 30.

Author: Bruce Amani