Gambia Wataka Kushiriki Kombe la Dunia 2026

39

Rais wa Shirikisho la Kandanda nchini Gambia (GFF) Lamin Kaba Bajo, ameweka wazi kuwa matamanio yao ni kuona timu ya taifa hilo inafuzu kucheza michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2026.

Bajo ametoa kauli hiyo baada ya timu ya taifa hilo “Nge” kukaa kwenye mkao wa kufuzu mashindano ya Afcon 2023 Ivory Coast ambayo itakuwa ni mara ya pili baada ya awali kushiriki Afcon Cameroon na kufika robo fainali.

“Malengo yetu yajayo ni kucheza Kombe la Dunia 2026, kwa kweli hilo ndiyo tunalifanyia kazi kwa sasa”, alisema Bajo.

Kombe la Dunia 2026 litafanyika kwa mataifa matatu kushirikiana Canada, Mexico na Marekani pia kutakuwa na ongezeko la timu ambazo zitashiriki mpaka 48.

Author: Asifiwe Mbembela