Horoya ya Guinea yamnyakua Enock Atta kutoka Azam

346

Timu ya Horoya ya Guinea imemsajili mchezaji Enock Atta Agyei siku chache baada ya kutangazwa kuachwa na klabu ya Azam FC ya Tanzania.

Atta anakuwa mchezaji wa tatu kutoka ligi ya Tanzania kusajiliwa na klabu hiyo baada ya Tafadzwa Kutinyu na Heritier Makambo. Ripoti kutoka nchini Guinea zilizochapishwa na gazeti la michezo la Mwanaspoti nchini Tanzania zinasema mchezaji huyo ametia kandarasi ya miaka mitano.

Nyota wengine walioachwa na Azam ni Ramadhan Singano, Obrey Chirwa, Steven Kingue, Danny Lwanga, Hassan Mwasapili na Joseph kimwaga.

Author: Bruce Amani