Koeman asema hana presha Barcelona

310

Kocha wa Fc Barcelona Ronald Koeman amesema hafikiri kama mchezo wa Ligi Kuu Hispania wa El Clasico baina yao na wapinzani Real Madrid unatakiwa kumfanya kuwa kwenye hofu.

Kocha Ronald Koeman ameyasema hayo wakati akizungumzia maandalizi ya Barca kuelekea mtanange wa Leo Jumapili Octoba 24, ambapo vijana wa Nou Camp watakuwa nyumbani kucheza na Real Madrid.

Itakumbukwa hofu ilikuwa imetawala vilivyo kuwa kocha huyo atafutwa kazi kufuatia matokeo mabovu akiwa anashika nafasi ya saba kwenye msimamo wa La Liga lakini Rais wa klabu Juan Laporta alisema “atabakia”.

“Kama kocha wa Barcelona nastahili kuwa na presha, ni timu kubwa inahitaji matokeo mazuri kila muda, lakini najua umuhimu wa El Clasico”, alisema Koeman.

Author: Bruce Amani