Leopards, Bandari FC Zafungana 2-2

150

AFC Leopards imelazimishwa sare ya bao 2-2 na Bandari FC katika mchezo wa Ligi Kuu nchini Kenya KPL mtanange uliopigwa dimba la Nyayo Leo Jumapili.

Leopards inayonolewa na Patrick Aussems ilikuwa inahitaji kushinda ili kutengeneza mazingira salama kwenye msimamo wa Ligi hiyo lakini haikuwa hivyo baada ya dakika tisini timu zikagawana alama moja moja.

Kwenye mechi hiyo magoli ya Bandari FC yamefungwa na wachezaji wawili wa Harambee Stars’ Abdallah ‘Starboy’ Hassan na Yohanna ‘Mbatizaji’ Mwita wakati yale ya kusawazishwa yamefungwa na kinda wa Ingwe Maxwell Otieno na Marvin Nabwire.

Kufuatia matokeo hayo, Bandari wanaketi nafasi ya nane na pointi 28 wakati Leopards wakiwa nafasi ya 10 na alama 26.

Author: Bruce Amani