Tetesi za Mastaa Ulaya: Manchester United yakubali kuondoka kwa Paul Pogba

231

Rais wa klabu ya Paris St-Germain Nasser al-Khelaifi amesema anaamini mshambuliaji wake raia wa Brazil Neymar Jr 28, na winga wa Kifaransa Kylian Mbappe 21, watabakia klabuni hapo kwa misimu mingi zaidi.

Chelsea ni miongoni mwa timu nne ambazo zinawania saini ya beki wa kati wa Bayern Munich David Alaba 28, klabu nyingine ni Barcelona, Real Madrid and PSG.

Manchester United wanahitaji kumuuza kiungo wao ghali Paul Pogba 27, baada ya kiungo huyo kusema hana furaha ndani ya klabu hiyo yenye masikani yake Old Trafford.

Real Madrid na Juventus zimekuwa zikihusishwa kuwania saini ya kiungo huyo raia wa Ufaransa, United hawana hofu juu ya kushindwana kwa bei yake.

Author: Bruce Amani