Wijnaldum aipeleka Uholanzi 16 bora Euro 2020

244

Bao la Memphis Depay na mawili ya kiungo mkabaji wa zamani wa Liverpool Georginio Wijnaldum yaipa uhakika wa asilimia 100 timu ya taifa ya Uholanzi kufuzu kucheza hatua ya 16 bora ya Euro 2020 baada ya kuitandika bao 3-0 Macedonia Kaskazini.
Kikosi cha kocha Frank de Boer kilikuwa kimefuzu hata kabla ya mchezo huo ambapo walishinda mbele ya Ukraine na Austria katika mechi za Kundi C zilizopigwa mwanzoni.
Wakiwa tayari wana uhakika wa kucheza hatua ya 16 bora, Uholanzi walionyesha kandanda safi mbele ya mashabiki 12,000 ambao walishuhudia mtanange huo katika dimba la Johan Cruyff.
Winga Depay anafunga bao hilo ikiwa ni siku chache tangu dili la kutua Barcelona kunoga vilivyo.
Kufuatia matokeo hayo, Uholanzi watasafiri kuwafuata wapinzani wao watakaomaliza nafasi ya tatu kwenye kundi D, E, au F mtanange utapigwa Juni 27.

Author: Bruce Amani