Barcelona Yasimama Kiuchumi

56

Barcelona imeingiza faida ya pauni milioni 86 kwa mwaka uliopita na sasa klabu hiyo inategemea kuingiza zaidi ya pauni milioni 240 kwenye kipindi cha mwaka mmoja ujao.

Miamba hiyo ya soka la Hispania msimu uliopita walishindwa kufanya usajili wowote kutokana na hasara waliyoingia kiasi cha kupoteza pauni milioni 422.

Kutokana na hasara pamoja na zuio la Fifa, Barcelona walichelewa hata kuwasajili wachezaji wake kwenye mfumo akiwemo staa wa Poland Robert Lewandowski na winga wa kimataifa wa Brazil Raphinha.

Barcelona wanategemea saizi watarejea kwenye mfumo mzuri kiuchumi pamoja na kufanya vizuri uwanjani.

Author: Bruce Amani