Bayern yatandikwa na Augsburg Bundesliga

Vinara wa Ligi Kuu nchini Ujerumani Bayern Munich wametandikwa goli 2-1 dhidi ya Augsburg mtanange uliopigwa Ijumaa Novemba 19.

Ushindi wa Augsburg unaifanya kukwea mpaka kuondoka kwenye mstari wa kushuka daraja licha ya Bayern kutawala mchezo huo kwa muda wote.

Magoli ya Mads Pedersen na Andre Hahn yaliipa uhakika wa ushindi kwenye dakika 45 za kwanza kqbla ya Robert Lewandowski kufunga moja la kufutia machozi.

Matokeo hayo yanahitimisha mechi nne mfululizo kushinda kwenye Ligi.

“Matokeo haya siyo sawa, nadhani Augsburg hawakupaswa kushinda” alisema kocha Julian Nagelsmann wa Bayern Munich.

Mchezo huo ulikuwa wa kihistoria kwa kiungo mshambuliaji wa Ujerumani Thomas Muller ambaye anafikisha mechi ya 600 ndani ya Bavaria hao.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends