Brazil yaifumua 1-0 Colombia kufuzu Kombe la Dunia Qatar 2022

649

Brazil inakuwa timu ya kwanza bara la America Kusini kufuzu Kombe la Dunia Qatar 2022 huku kukiwa na mechi nyingi mkononi, pia takribani mwaka mzima kabla ya kuanza kwa fainali hizo.

Licha ya kufuzu, Brazil wamevuna alama tatu nyingine mbele ya Colombia baada ya kuibuka na ushindi wa goli 1-0 bao pekee likifungwa na Lucas Paqueta akimalizia pasi murua ya kiungo mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar Jr.

Matokeo hayo yanaifanya Brazil kuongoza msimamo kwa tofauti ya alama 18 wakati timu inayofuatia ikiwa ni Chile nafasi ya nne.

Timu nne za juu kwenye msimamo barani Amerika Kusini hufuzu moja kwa moja kwenda Kombe la Dunia.

Author: Bruce Amani