Bye Bye Azam, Sure Boy

250

Azam FC imemuaga kiungo wake Salum Abubakary ‘Sure Boy’, baada ya kuthibitisha kusitisha mkataba wake Jana Jumanne Disemba 21, 2021.

Azam Fc imemuaga kiungo huyo anayetajwa kujiunga na Young Africans katika kipindi hiki cha Dirisha Dogo la Usajili, kwa kuweka taarifa maalum kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Taarifa hiyo imeeleza: “Salum Abubakary, alasiri ya leo Disemba 22, amekuja Azam Complex kuchukua barua yake ya kuruhusiwa kuondoka Azam Football Club (Release Letter).”

Herry Mzozo: Sure Boy amesaini Young Africans
“Amekabidhiwa barua hiyo na afisa mtendaji mkuu, Abdulkarim Amin Popat.”

“Kwa barua hiyo, ni rasmi sasa kwamba Salum Abubakary siyo tena mchezaji wa Azam Football Club.”

Salum Abubakary ‘Sure Boy’ alikua sehemu ya wachezaji wachache Waandamizi wa Azam FC, ambao walikua wamesalia klabuni hapo baada ya kuondoka kwa Mshambuliaji John Raphael Bocco.

‘Sure Boy’ alisimamishwa Azam FC kwa kosa la utovu wa nidhamu miezi minne iliyopita, sambamba na wachezaji wengine Mudathir Yahya na Agrey Morris

Author: Asifiwe Mbembela