Yanga yapanga ujenzi wa uwanja Kigamboni

608

Senzo Masingiza Mbatha, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Timu ya Wananchi Yanga ameweka wazi kuwa mradi wao wa ujenzi wa Uwanja ambao unafahamika kwa jina la Kigamboni Complex ‘Home of Champions’ tayari umeshawapata wakandarasi ambao wataanza kazi muda wowote kuanzia sasa.

Senzo ameanika wazi mpango huo, ikiwa ni siku chache tangia mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Simba kutangaza mchakato wa kuchangisha fedha za ujenzi wa Uwanja wa kisasa ambao utagharimu Shilingi Bilioni 30.

Senzo amesema: “Mradi tayari ulishapata wakandarasi wa kuuanza kufanya kazi ambapo muda wowote kuanzia sasa Kigamboni Complex Home of Champions itaanza kufanyiwa kazi jambo ambalo ni maendeleo makubwa kwa klabu yetu.

“Yanga tuna mipango mingi sana endelevu na bora kwa ajili ya klabu hivyo kuna vitu vingi sana vinatakiwa kukamilika ili watu waone maendeleo yenyewe,”amesema kiongozi huyo.

Author: Asifiwe Mbembela