Dube aua kwa Mkapa, Kocha mpya Yanga aanza na kipigo

322

Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Yanga wameanza vibaya chini ya kocha mpya Naslideine Al Nabi ambaye unakuwa mchezo wake wa kwanza akichukua kijiti cha Cedric Kaze.

Kwenye mechi hiyo iliyopigwa dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam Yanga wamepoteza kwa kufungwa bao 1-0 na Azam, bao la jioni kabisa.

Kipindi cha Kwanza timu zote zilitoshana nguvu na kuwafanya waende vyumba vya kubadilishia nguo ubao ukisoma Yanga 0-0 Azam FC.

Ni Prince Dube dakika ya 85 alipachika bao la ushindi nje ya 18 huku akiwa zaidi ya mita 35 baada ya kuwazidi maarifa walinzi wa kati wa Timu ya Wananchi.

Kocha Al Nabi kabla ya kutua Yanga alikuwa kocha huru baada ya kufutwa kazi na EL Merreikh ya Sudan mwezi Machi kutokana na kutokuwa na mwelekeo kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.

Ushindi huu unaifanya Azam FC kulipa kisasi cha kupoteza mchezo wa raundi ya kwanza dhidi ya Yanga, mchezo uliopigwa Azam Complex.

Author: Asifiwe Mbembela