Kikosi Cha Kenya Kuikabili Iran mechi ya Kirafiki

116

Kocha Mkuu wa kikosi cha timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars, Engin Firat ametaja majina ya wachezaji 24 watakaounda kikosi kitakachokuwa na mchezo wa kirafiki dhidi ya Iran utakaopigwa Jumanne ya wiki ijayo.

Kwenye kikosi hicho, amejumuishwa Masud Juma, ambaye awali ilionekana angekosa mchezo kutokana na majeruhi hata hivyo vipimo vya mwisho kimeonyesha kwamba anaweza kucheza.

Pamoja na Juma kuwa sehemu ya kikosi, Benson Omala atashuhudia mtanange huo akiwa nyumbani kufuatia kutojumuishwa kwake ingawa ndiye kinara wa kupachika mabao KPL.

Kwenye kikosi cha mwisho kimeundwa na makipa watatu, walinzi nane, viungo tisa na washambuliaji wanne.

Makipa

Patrick Matasi, Ian Otieno, Bryne Odhiambo

Walinzi
Daniel Sakari, Eric Ouma, Johnstone Omurwa, David Ochieng, Brian Mandela, Joseph Okumu, Daniel Anyembe, Abud Omar

Viungo

Amos Nondi, Wilkims Ochieng, Richard Odada, Alpha Onyango, Duke Abuya, Teddy Akumu, Kenneth Muguna, Victor Omune, Abdallah Hassan

Washambuliaji

Elvis Rupia, Alfred Scriven, Michael Olunga, na Masud Juma

Author: Bruce Amani