Lewandowski afikia rekodi ya miaka 42

172

Mshambuliaji wa kimataifa wa Poland Robert Lewandowski ameifikia rekodi ya mshambuliaji wa zamani wa Bayern Munich Gerd Muller kwa kufunga goli katika kipindi kimoja cha msimu wa Kandanda.

Lewandowski ameifikia rekodi hiyo wakati Bayern Munich ikiichapa bao 5-0 Stuttgart mtanange uliopigwa Leo Jumanne Disemba 14, 2021.

Lewandowski aliingia kambani mara mbili kwenye mechi hiyo likiwa ni bao la 42 kwa msimu huu wa 2021 akifikia rekodi ya Muller ya mwaka 1972 (42) huku mabao mengine yakifungwa na Serge Gnabry ambaye amefunga bao tatu (hat-trick).

Endapo Lewandowski atafunga kwenye mechi ya ijumaa dhidi ya Wolfsburg itamfanya mchezaji huyo kutengeneza rekodi yake mwenyewe.

Matokeo hayo yanaifanya Bayern kutengeneza tofauti ya alama tisa tofauti ya timu iliyonafasi ya pili Borrusia Dortmund ambao wanaweza kupunguza alama mpala sita endapo watashinda mchezo wao dhidi ya Greuther Furth.

Author: Asifiwe Mbembela