JKT Tanzania wapigishwa kwata na Simba

296

Simba Sc imefanikiwa kwenda raundi ya nne ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC) baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya JKT Tanzania inayoshiriki Ligi daraja la kwanza.

Ushindi wa Simba umetokea katika dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, mtanange uliopigwa Leo Jumanne Disemba 14, 2021.

Bao pekee kwenye mechi hiyo ya kwanza baada ya Wekundu wa Msimbazi Simba kutoka kwenye mtanange wa Dabi ya Kariakoo, limefungwa na kiungo mshambuliaji wa zamani wa Mbeya City Kibu Dennis Prosper kunako dakila ya 27 ya mchezo ungwe ya kwanza.

Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Kombe hilo, kwa mjibu wa Barbara Gonzalez Mtendaji Mkuu wa Simba wakati anamtambulisha kocha Franco Martin alisema moja la lengo la kulitimiza ni kutetea taji la ASFC.

Author: Asifiwe Mbembela