Mayele Atamba Afrika

433

Fowadi wa Yanga Fiston Kalala Mayele ametangazwa na Shirikisho la soka nchini kuwa mshindi wa bao bora. Bao lake dhidi ya US Monastir katika uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam lilipigiwa kura kuwa bao bora la msimu.

Kwenye mchezo ule, Yanga walishinda bao 2-0 ambapo bao moja alilifunga mshambuliaji wa Musonda pamoja na bao la Mayele.

Yanga iliibamiza Monastir 2-0 Machi 19, bao lingine akifunga Kennedy Musonda katika mchezo wa Kundi D Kombe la Shirikisho Afrika.

Author: Asifiwe Mbembela