Msuva Aichapa Uganda Kufuzu AFCON 2023

152

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Saimon Msuva ameipa ushindi timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kwa kufunga bao pekee kwenye mchezo wa tatu kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa Bingwa Afrika AFCON nchini Ivory Coast dhidi ya Uganda.

Taifa Stars wamevuna alama hizo tatu kwenye mchezo uliochezwa katika mji wa Ismailia, Misri ambapo Msuva nyota wa zamani wa Yanga, Difaa el Jadida na Wydad Casablanca alikwamisha mpira nyavuni akitumia pasi ya Dickson Job.

Linakuwa ni bao la tatu mfululizo kwa Msuva anayekipiga kunako klabu ya Al-Qadsiah ya Saudi Arabia kufunga dhidi ya Uganda kwenye mashindano yote, moja ya rekodi nzuri kwake.

Kwa matokeo hayo, Stars wanafikisha alama nne kwenye mechi tatu ambapo sasa watarudiana na Uganda Machi 28 mwaka huu uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Author: Asifiwe Mbembela