Mbeya City yaichapa Dodoma Jiji 2-0

418

Timu ya kizazi kipya, Mbeya City imeibuka na ushindi mnono wa goli 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara mtanange uliopigwa dimba la Kumbukumbu ya Sokoine Jijini Mbeya Leo Jumatatu Disemba 6.

Mbeya City ambao misimu miwili iliyopita walikuwa wanasubiri neema ya michezo ya mtoano kubakia kwenye Ligi Kuu, wanaonekana msimu huu wameimarika kiasi kutokana na ushindi na matokeo ambayo wamekuwa wakiyapata.

Mabao ya Mbeya City leo yamefungwa na Hussein Masalanga dakika ya 42 na Paul Nonga dakika ya 88 na kwa ushindi huo timu hiyo inafikisha pointi 14.

Matokeo hayo yanaifanya Mbeya City kukwea mpaka nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakati Dodoma Jiji inabakiwa na alama 12 ikishika nafasi ya tano baada ya mechi nane.

Author: Asifiwe Mbembela