Mtibwa Sugar yaichapa Kagera Sugar

408

Kwa mara ya kwanza baada ya mechi nane kikosi cha Mtibwa Sugar kimepata ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Kagera Sugar mchezo ambao ulikuwa ni Dabi ya Sukari uliopigwa dimba la Jamhuri Morogoro.

Mtibwa Sugar ikicheza nyumbani mkoani Morogoro imejihakikishia ushindi huo wa kwanza msimu huu, kupitia kwa bao la Riphat aliyepachika bao hilo pekee kunako dakika ya 13.

Mtibwa Sugar ilikua haijapata ushindi katika michezo saba iliyopita, hali ambayo iliifanya klabu hiyo Kongwe katika Ligi Kuu kuburuza mkia.

Ushindi huo unaiwezesha Mtibwa Sugar kufikisha alama 5, ambazo zinaendelea kuwaweka mkiani mwa msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Author: Asifiwe Mbembela