Simba Full Mkoko Kuivaa Yanga

348

Kaimu Afisa Habari wa klabu ya Simba Ally Sharty “Babu Chiko” amesema hakuna mchezaji ambaye ni majeruhi kuelekea mtanange wa Watani wa Jadi Yanga mechi itakayopigwa dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam Disemba 11.

Simba ambayo inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, imesema kuwa kwa sababu haina majeruhi inaamini kuwa itashinda na kwenda kuongoza msimamo wa NBC League.

Akizungumza na Wanahabari Ally Sharty ‘CHIKO’, amesema maandalizi ya mchezo huo yalianza tangu Jumatatu (Desemba 06) mjini Lusaka-Zambia, na leo Jumatano (Desemba 08) jioni kitaendelea na mazoezi baada ya kuwasili Jijini Dar es salaam juzi Jumanne (Desemba 07) majira ya usiku.

“Tunaamini mchezo huu utaturudisha kwenye nafasi yetu, tumeshazoea kuwatanguliza ndugu zetu, na ndivyo ilivyo kwa msimu huu,”

“Kikosi kilianza maandalizi ya mchezo huu tangu Jumatatu (Desemba 06) kikiwa mjini Lusaka-Zambia, na leo Jumatano (Desemba 08) kitaendelea na mazoezi baada ya kuwasili nchini Jana Jumanne (Desemba 07).” amesema Sharty

Mchezo wa mwisho dhidi ya Young Africans, Simba Sc ilipoteza kwa kufungwa 1-0, bao likifungwa na Mshambuliaji kutoka DR Congo Fiston Kalala Mayele.

Author: Asifiwe Mbembela