Sogne kuikosa Simba katika Debi ya Kariakoo

451

Mshambuliaji Yacouba Sogne atakuwa mchezaji pekee kwa upande wa Yanga atakayekosa mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara wa Watani wa Jadi dhidi ya Simba utakaopigwa dimba la Mkapa Jijini DSM Disemba 11, 2021.

Yanga ambayo inatakua mgeni wa jina katika mchezo huo imetanabaisha hilo kupitia idara yake ya Habari na Mawasilino inayoongozwana Hassan Bumbuli.

“Tumejiandaa kushinda mchezo huo, mpaka sasa kikosi chetu kipo vizuri na hadi nakuja hapa taarifa nilizozipata kutoka kambini wachezaji wote wapo katika hali nzuri isipokua Yacoub Sogne, ambaye ni Majeruhi,” alisema Bumbuli.

“Dhamira yetu ni kupata matokeo ambayo yatatuongezea nafasi ya kulisogelea Taji la Ligi Kuu ambalo tumelikosa kwa muda mrefu, tunaamini msimu huu Taji hili lina kila sababu ya kurudi nyumbani.” amesema Bumbuli

Yanga inaingia kwenye mechi hiyo ikijua wazi kuwa ushindi utaipa utanuzi wa msimamo wa Ligi na kufikia tofauti ya alama sita wakati wakipoteza wataachwa kwa alama moja.

Author: Bruce Amani