Simba Wachechemea kwa Mtibwa Sugar

385

Wekundu wa Msimbazi Simba wameambulia alama moja katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara mbele ya wenyeji Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi uliopigwa dimba la Manungu Turiani mkoani Morogoro Leo Jumamosi Januari 22.

Mtibwa Sugar inafikisha pointi 12 katika mchezo wa 13 na kusogea nafasi ya 13, wakati Simba SC inafikisha pointi 25 katika mchezo wa 12, ingawa inabaki nafasi ya pili, ikizidiwa pointi saba na watani wa jadi, Simba baada ya timu zote kucheza mechi 12.

Kwingineko, Azam FC imeibuka na ushindi mnono wa goli 4-0 dhidi ya Tanzania Prisons kwa mabao ya Tepsi Evance dakika ya 27, Ismail Aziz Kader dakika ya 68, Ibrahim Ajibu dakika ya 70 na Justin Zullu dakika ya 82 Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga mkoani Rukwa.

Nao Biashara United imelazimishwa sare ya bila kufungana na Geita Gold Uwanja wa Karume mjini Musoma mkoani Mara.

Azam FC inafikisha pointi 21 na kusogea nafasi ya nne, ikizidiwa pointi moja na Mbeya City baada ya timu zote kucheza mechi 13, wakati Tanzania Prisons inabaki na pointi zake 11 za mechi 13 na sasa inahamia mkiani.

Biashara United inafikisha pointi 11 katika mechi ya 13 nafasi ya 14 na Geita Gold sasa ina pointi 14 za mechi 13 pia nafasi ya 10.

Author: Asifiwe Mbembela