Tetesi za Mastaa Ulaya: Gabriel Jesus, Mahrez, Silva wawekwa chambo Man City, Mbappe aendelea kushinikiza kuondoka PSG

169
Manchester City wanajiandaa kuwatoa wachezaji watatu ambao ni mshambuliaji wa Brazil Gabriel Jesus, 24, nahodha wa Algeria Riyad Mahrez, 30, kiungo wa Ureno Bernardo Silva, 26, kwa ajili ya kumsajili strika matata wa Tottenham Hotspur Harry Kane 27.

Dili hilo likifanikiwa Kane atakuwa anaingiza kiasi cha pauni 400,000 kwa wiki ndani ya Manchester City, ingawa Mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy alipinga mauzo hayo.
Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Kylian Mbappe 22, amepanga kukataa ofa ya mkataba mpya wa klabu ya Paris St-Germain akishinikiza kuondoka klabuni hapo na kujiunga na miamba ya soka la Hispania Real Madrid.
Paul Pogba 28, anaweza kung’oka klabuni Manchester United kufuatia kugoma kumwaga wino wa pauni 350,000 kwa wiki, na Man United haiko tayari kumuachia kuondoka bure msimu ujao baada ya kandarasi yake kumalizika.
Manchester United pia inaendelea kupambana kupata saini ya beki wa kati wa Real Madrid Raphael Varane 28, Madrid wanahitaji pauni milioni 50 wakati United wako tayari kutoa pauni milioni 40.

Author: Bruce Amani