Vinara AC Milan waduwazwa na Atalanta, wazabwa 3-0 nyumbani San Siro

157

Uongozi wa AC Milan kileleni mwa Serie A umepunguzwa kwa pointi mbili baada ya kuonyeshwa kandanda na Atalanta dimbani San Siro kwa kufungwa 3 – 0. Cristian Romero alifunga bao la kichwa kutokana na kona ya Robin Gosens baada ya dakika ya 26 kabla ya Josip Ilicic kuangushwa kwenye kisanduku na Frank Kessie wa Milan katikati ya kipindi cha pili. Illicic alifunga penalty hiyo kabla ya Duvan Zapata kuongeza la tatu baadae

Inter Milan wangetoshana pointi kileleni kama wangeshinda leo, lakini wakakabwa sare tasa na Udinese. Atalanta ambao ndio timu ya pili pekee kuifunga AC Milan msimu huu wamepanda hadi nafasi ya nne.

Author: Bruce Amani