AC Milan yaitungua Cagliari 2-0 na kuendelea kushika usukani wa Serie A

275

AC Milan imeendelea kuketi kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu nchini Italia Serie A baada ya kuandikisha ushindi wa goli 2-0 dhidi ya Cagliari katika mchezo uliopigwa Jana Jumatatu.

Mshambuliaji wa timu hiyo mkongwe Zlatan Ibrahimovic aliingia kambani mara mbili na kuvuna alama tatu ambapo sasa wanafikisha 43 na kujitenga na Inter Milan wenye alama 40.

Goli la kwanza kwa Ibrahimovic, alifunga kwa njia ya penati kabla ya lile la pili lililofungwa kunako dakika ya 52 na sasa anafikisha goli 13 katika mechi 13.

Author: Asifiwe Mbembela