Yanga yaibwaga Simba Kombe la Mapinduzi katika fainali

410

Yanga imeibuka na ubingwa wa Kombe la Mapinduzi kwa ushindi wa penalti 4-3 dhidi ya Simba baada ya dakika 90 kukamilika sare tasa.

Nyota wa mchezo huo ni Farouk Shikalo ambaye aliokoa penalti moja ya Joash Onyango na Meddie Kagere kugongesha mwamba penalti yake moja.

Saido Ntibanzokiza ambaye alikuwa msumbufu ndani ya dakika zote 90 amesema kuwa wachezaji wenzake walimuomba awape sapoti naye akasema kwamba hana tatizo atafanya kazi.

Alifunga penalti ya mwisho iliyomshinda mlinda mlango Beno Kakolanya ambaye hakuwa na namna baada ya kuokoa matukio matano ya hatari dani ya dakika 90.

Huu unakuwa ni ubingwa wa pili kwa Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze mara yao ya mwisho ilikuwa mwaka 2007 huku Simba ikibakiwa na mataji yake matatu ndani ya kabati lao.

Author: Asifiwe Mbembela