Bye Bye Mukoko Tonombe Yanga

455

Klabu Yanga imetangaza kuachana rasmi na aliyekuwa kiungo mkabaji wa timu hiyo Tonombe Mukoko baada ya kuitumikia kwa walau misimu miwili.

Yanga imeachana na mchezaji huyo kwa kile ambacho kinaelezwa kuwa kumefanyika mabadilishano ya wachezaji, ambapo Timu ya Wananchi imemchukua Chiko Ushindi wakati Tonombe akielekea TP Mazembe.

Taarifa ya Yanga jioni hii imemshukuru Mukoko kwa mchango wake kama Nahodha Msaidizi kwa kipindi cha msimu mmoja na nusu tangu awasili kutoka AS Vita ya kwao, Kinshasa.

Mukoko anakwenda Mazembe wiki moja baada ya Yanga kumsajili Mkongo mwingine, winga Chico Ushindi kutoka klabu hiyo ya Lubumbashi.

Author: Asifiwe Mbembela