Djuma Kapigwa Rungu na Bodi ya Ligi

223

Mlinzi wa kulia wa klabu ya Yanga Shaban Djuma amefungiwa kucheza mechi tatu na kutozwa faini ya Shilingi 1,000,000 kwa kumpiga kiwiko mchezaji wa Polisi Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu baina ya timu hizo.

Taarifa ya Bodi ya Ligi ya Shirikisho la Soka Tanzania (TPLB) iliyotolewa Leo Ijumaa Januari 28, 2022 imesema kwamba pamoja na mchezaji huyo, katika mechi hiyo mwamuzi wa kati Hance Mabena na wasaidizi wake, Paschal Joseph na Jackson Samuel wote wameondolewa kwenye orodha ya waamuzi wa Ligi Kuu kwa mechi tatu hadi tano kwa kutochukua hatua dhidi ya tukio hilo.

Waamuzi wasaidizi wamepewa adhabu hiyo kwa kile ambacho kinaelezwa kuwa walishindwa kumtafsiri tukio hilo.

Author: Asifiwe Mbembela