Uefa yaahirisha mashindano ya Ligi ya Mabingwa na Europa

Shirikisho la soka Ulaya UEFA leo limetangaza maamuzi magumu kuhusiana na michuano ya UEFA Champions League na UEFA Europa League wakati huu wa mlipuko wa virusi vya corona.

UEFA wametangaza kuahirisha michuano yote hiyo kwa muda usiojulikana kutokana na mlipuko wa virusi vya corona kuendelea kushika kasi.

Licha ya kuwa imesimamishwa michuano hiyo kwa muda usiojulikana lakini inaripotiwa kuna inaweza kuendelea Julai au Agosti 2020 mwaka huu.

Hii pia ni kupisha Ligi za ndani ziweze kumalizika na kuangalia maambukizi ya corona kama yatakuwa yamepungua, itakumbukwa pia Euro 2020 imefutwa, Tokyo Olympic imefutwa kutokana na janga la virusi vya Corona.

Author: Bruce Amani

Share With Your Friends