Cameroon kuandaa fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika

393

Cameroon imechaguliwa hii leo kuwa mwenyeji wa mechi ya fainali ya klabu bingwa wa soka barani Afrika, itakayochezwa mwezi Mei mwaka huu. Shirikisho la soka la Afrika limesema uwanja wa Japoma mjini Douala utaiandaa mechi hiyo tarehe 29 Mei.

Itakuwa fainali ya kwanza baada ya kuanzishwa kwa mfumo wa mtoano katika mechi moja tu, tofauti na zamani ambapo timu zilicheza mechi mbili, moja nyumbani, na nyingine ugenini.

Mfumo huo wa zamani ulibadilishwa baada ya ghasia zilizoikumba mechi ya pili kati ya klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco na Esperance ya Tunisia.

Katika mechi hiyo, Wydad Casablanca walikataa kuendelea kucheza baada ya goli lao kukataliwa, huku kukiwa hakuna utaratibu wa video wa kuamua utata. Bado malalamiko kuhusiana na mechi hiyo yako katika mahakama ya michezo mjini Lausanne, Uswisi.

Author: Bruce Amani