Dortmund yavuna ushindi mnono, Bayern yakabwa sare

202

RB Leipzig imeendelea kuwa kileleni mwa msimamo wa Bundesliga baada ya kulazimisha sare ya goli 1-1 na Mabingwa wa Ligi hiyo Bayern Munich kwenye mchezo uliochezwa siku ya Jumamosi.

Goli 5 kwenye mechi 4 kwa mshambuliaji wa Bayern Munich Roberto Lewandowski akiwa amefunga goli moja katika mchezo huo kabla ya kusawazishwa kupitia kwa Emil Forsberg.

Tangu msimu huu kuanza, Bayern imekuwa ikipata tabu kupata matokeo chacha licha ya kuwa na maingizo mapya kama Phillipe Coutinho aliyejiunga na timu hiyo kutokea Fc Barcelona.

Licha ya sare hiyo lakini mchezo huo kuwa na kasi kubwa kwa dakika tisini timu zikigawana vipindi zaidi ingawa mechi ilionekana kuwa upande wa Bayern Munich.

Wakati Munich wakitoa sare dhidi ya Leipzig, wapinzani wao Borussia Dortmund wamefanikiwa kurejesha makali yao baada ya kuitandika Bayern 04 Leverkusen kwa goli 4-0.

Marcus Reus mshambuliaji wa Dortmund akifunga goli 2 katika ushindi huo huku goli nyingine zikifungwa na Paco Alcacer na Raphael Guerreiro 83′

Msimamo unaonyesha kuwa Leipzig wanashika nafasi ya kwanza kwa alama 9 wakati Bayern Munich na Dortmund wakiwa nafasi ya pili na alama 8 Wolfsburg nafasi ya nne.

Author: Bruce Amani