Faisal Salum ajifunga pingu kuendelea kuitumikia Yanga SC

739

Kiungo mkabaji wa Kizanzibar Feisal Salum ‘Fei Toto’ ameongeza kandarasi ya miaka minne ya kukitumikia kikosi cha Young Africans Sports Club baada ya mkataba wake kutajwa kuelekea kumalizika.

Akiwa katika picha ya pamoja na Injinia Hersi Said Mkurugenzi wa Uwekezaji kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Klabu hiyo amesema kuwa ameongeza mkataba wa miaka minne ili kuendelea kuwatumikia wananchi.

Hivyo, Fei Toto atakuwa ni mali ya Yanga mpaka 2024 kwa timu itakayokuwa inasaka saini yake lazima ijipange kuweka mkwanja mezani.

Kwa msimu wa 2019/20, Feisal amekuwa bora ndani ya Ligi Kuu Bara akianza kikosi cha Kwanza kwenye jumla ya mechi 22.

Msimu uliomalizika wa 2019/20  tuzo moja ya mchezaji bora wa msimu ndani ya Yanga aliyokabidhiwa na wadhamini wakuu wa Klabu hiyo, kampuni ya SportPesa.

Amefunga bao moja ndani ya ligi msimu huu katika Uwanja wa Mkapa dhidi ya Mwadui FC kwenye sare ya kufungana bao 1-1, ambapo pia kwenye kombe la FA ana goli moja akifunga katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Simba SC

Feisal alisaini mkataba wa miaka mitatu wakati akijiunga na Yanga mwaka 2018 akitokea JKU ya Unguja, hivyo mkataba wake ulitakiwa umalizike mwaka 2021 na sasa ameongeza kandarasi juu yake.

Author: Asifiwe Mbembela