Jack Grealish atajwa kikosi cha England cha kocha Southgate kwa mara ya kwanza

374

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya England amewaita kwenye kikosi chake wachezaji watatu wakiwa mbadala wa wale walioachwa nje kutokana na majeruhi. Kiungo mshambuliaji wa Aston Villa Jack Grealish amekuwa miongoni mwa majina ambayo yamejumuishwa katika muito huo wa kocha Gareth Southgate na kuwa mara ya kwanza kwa kiungo huyo kuitwa katika timu ya wakubwa ya England.

Hata hivyo, Marcus Rashford na Harry Winks wametolewa nje katika kikosi hicho kinachojiandaa na mchezo dhidi ya Iceland na Denmark ya National League. Grealish, 24, amewai kuiwakilisha England katika timu ya wachezaji wa umri wa chini ya miaka 21 na alikuwa sehemu ya timu mwaka 2016. Wachezaji wengine ni Conor Coady wa Southampton na beki wa Arsenal Ainsley Maitland-Niles.

Kikosi cha Southgate kitacheza dhidi ya Iceland Septemba 5 baada ya hapo kitacheza mechi nyingine dhidi ya Denmark siku tatu baadae.

Kikosi cha England

Makipa: Dean Henderson, Jordan Pickford, na Nick Pope.

Walinzi: Trent Alexander-Arnold, Conor Coady, Eric Dier, Joe Gomez, Michael Keane, Ainsley Maitland-Niles, Tyrone Mings, Kieran Trippier, na Kyle Walker.

Viungo: Phil Foden, Mason Mount, Kalvin Phillips, Declan Rice, James Ward-Prowse, na Jack Grealish.

Mafowadi: Tammy Abraham, Mason Greenwood, Danny Ings, Harry Kane, Jadon Sancho, na Raheem Sterling.

Author: Asifiwe Mbembela