Kutazama mtanange kati ya Simba na Yanga 7,000

296

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara imethibitisha kuwa takribani tiketi 13,782 pekee zitauzwa kwa mashabiki na wadau wa soka katika mtanange Na. 208 wa Ligi Kuu ya Vodacom 2020/2021 baina ya Simba Sc na Young African Sc utakaopigwa Julai 3, 2021, Dimba la Benjamin Mkapa, Jijini Dar es Salaam.

Kupitia taarifa rasmi iliyotolewa Leo Jumatatu Juni 28 na Kitengo cha Habari na Mawasiliano cha TPLB kimesema maamuzi hayo yamefikiwa kufuatia mchezo uliokuwa umepangwa kupigwa awali Mei 8 kuota mbawa huku mashabiki wakiwa wamelipia viingilio vya mechi kutokana na sintofahamu ya mabadiliko ya muda wa mechi.

Hatua hiyo imekuja baada ya maamuzi yaliyofanywa awali kuhusu washabiki ambao walikata tiketi kwa ajili ya mchezo ambao uliahirishwa Mei 8, 2021 (Simba SC dhidi ya Young Africans SC), kuruhusiwa kutumia kadi zao (NCARD) kuingia uwanjani bila kulazimika kulipia tena tiketi kwa ajili ya mchezo wa Julai 3.

Katika tiketi 13,782 zitakazouzwa, tiketi 2,218 ni za jukwaa la kijani (mzunguko), tiketi 11,280 ni za jukwaa la machungwa (Orange) na tiketi 284 za VIP B.

Bodi ya Ligi imesema hakutokuwa na tiketi za VIP A na VIP C zitakazouzwa kwa ajili ya mchezo huo wa Julai 3.

Gharama za tiketi zitakazouzwa ni kama ifuatavyo;-
Mzunguko – Tsh. 7,000
Machungwa – Tsh. 10,000
VIP B – Tsh. 20,000

Author: Asifiwe Mbembela