Simba kumenyana na Vital’O ya Burundi kilele cha Wiki ya Simba

415

Klabu ya Simba inatarajiwa kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Klabu Vital’O FC ya kutoka Burundi katika mchezo ambao unahitimisha siku saba za “Wiki Ya Simba”. Mchezo hui utapigwa Uwanja wa Mkapa, majira ya saa 11:00 jioni. Simba ambao ni mabingwa wa ligi kuu, kombe la FA na Ngao ya Jamii kwa msimu uliopita hutumia wiki ya Simba kufanya shughuli mbalimbali za kijamii kama kufanya usafi, kujitoa damu na shughuli kama hizo.

Katika miaka ya nyuma kabla ya huu wa 2020, siku ya kilele ilikuwa inafanyika Agosti 8, lakini mwaka huu kumekuwa na mabadiliko ya ratiba ambayo imechagizwa na maambukizi ya Virusi vya Corona. Hata hivyo siku ya kilele huwa rasmi kwa ajili ya kuwatambulisha wachezaji wapya na wale wa zamani ambao hutumika kwa msimu ujao. Miongoni mwa wachezaji wapya ni pamoja na Bernard Morrison, Larry Bwalya, Charles Ilanfya huku wale wa zamani ikiwa ni pamoja Ibrahim Ajibu, Said Ndemla, Meddie Kagere, John Bocco

Author: Asifiwe Mbembela