Mane, Salah wawania tuzo ya Ballon d’Or

147

Orodha ya wachezaji 30 wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa kandanda mwaka wa 2018 ya Ballon dOr imetolewa. Orodha hiyo imetawaliwa na washindi wa Ligi ya Mabingwa Ulaya Real Madrid, ambao wana wana wachezaji wanane walioteuliwa.

Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale na mshabuliaji wa England Harry Kane ni miongoni mwa walioteuliwa. Eden Hazard wa Chelsea, Mo Salah wa Liverpool na Kevin de Bruyne wa Manchester City ni miongoni mwa wachezaji 11 wa Premier League ya England waliotangazwa.

Washambuliaji wa Liverpool Mane na Salah

Tuzo ya Ballon d’Or, ilitolewa kwa mara ya kwanza mwaka wa 1956, kw akupewa mchezaji bora wa mwaka.

Sherehe ya kumtangaza mshindi wa tuzo hiyo ya kifahari itafanyika Paris Desemba 3, katika wakati ambao tuzo hiyo kwa upande wa wanawake itatolewa kwa mara ya kwanza.

Sergio Aguero wa Manchester City anawania pamoja na kipa Liverpool Alisson na mshambuliaji Sadio Mane na Roberto Firmino.

Paul Pogba, wa Manchester United, N’Golo Kante wa Chelsea na kipa wa Tottenham Hugo Lloris pia wako ndani.

Nyota wa Ureno Cristiano Ronaldo aliyeshinda tuzo hiyo mwaka uliopita pamoja na mshindi mara tano wa tuzo hiyo Lionel Messi pia wanawania

Orodha kamili:

2018 Ballon d’Or nominees
Position Country Club
Sergio Aguero Forward Argentina Manchester City
Alisson Goalkeeper Brazil Liverpool
Gareth Bale Forward Wales Real Madrid
Karim Benzema Forward France Real Madrid
Kevin de Bruyne Midfielder Belgium Manchester City
Edinson Cavani Forward Uruguay Paris St-Germain
Thibaut Courtois Goalkeeper Belgium Real Madrid
Roberto Firmino Forward Brazil Liverpool
Diego Godin Defender Uruguay Atletico Madrid
Antoine Griezmann Forward France Atletico Madrid
Eden Hazard Forward Belgium Chelsea
Isco Midfielder Spain Real Madrid
Harry Kane Forward England Tottenham
N’Golo Kante Midfielder France Chelsea
Hugo Lloris Goalkeeper France Tottenham
Mario Mandzukic Forward Croatia Juventus
Sadio Mane Forward Senegal Liverpool
Marcelo Defender Brazil Real Madrid
Kylian Mbappe Forward France Paris St-Germain
Lionel Messi Forward Argentina Barcelona
Luka Modric Midfielder Croatia Real Madrid
Neymar Forward Brazil Paris St-Germain
Jan Oblak Goalkeeper Slovenia Atletico Madrid
Paul Pogba Midfielder France Manchester United
Cristiano Ronaldo Forward Portugal Juventus
Ivan Rakitic Midfielder Croatia Barcelona
Sergio Ramos Defender Spain Real Madrid
Mohamed Salah Midfielder Egypt Liverpool
Luis Suarez Forward Uruguay Barcelona
Raphael Varane Defender France Real Madrid

Author: Bruce Amani